Dr Peter amesema biashara ya hewa ukaa ni muhimu Sana kwani inasaidia kwa kiasi kikubwa katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ambako watu wataachana kupika kupitia kuni na mkaa kwa kiwango kikubwa.
Watanzania walio wengi wanapika kwa kutumia kuni na mkaa ndio maana taasisi ya Cookfund wamesajili miradi ipatayo42 ya hewa ukaa na wamewezesha wataalamu 80 kwenye sekta 4 kwaajili ya kuwapa mafunzo ya matumizi ya hewa ukaa mpaka sasa washatoa semina6 za kuwajengea uwezo wataalam mbalimbali .
Lengo kubwa watu waingie kwenye biashara ya hewa ukaa ili kuzinusulu na kuziokoa ekta 48.14 milioni za misitu nchini Tanzania zisialibiwe kwa kukatwa.
Pia taasisi yao inatoa mafunzo kwa wakulima namna ya kutumia nishati safi ya kupikia ili wailing na kuitunza misitu yao na waingie kwenye biashara ya hews ukaa ambako itawasaidia kujiinua kiuchumi.
Habari picha na Ally Thabit
No comments:
Post a Comment