Monday, 13 May 2024

RAIS DR SAMIA KUONGOZA MKUTANO NCHINI UFARANSA


 Waziri wa Mambo Ya Nje na Ushilikiano wa Afrika Mashariki January Makamba amesema rais Dr Samia anaenda nchini  Ufaransa kwaajili ya kuongoza mkutano wa kujadili matumizi ya nishati safi ya kupikia ambako rais Dr Samia yeye ndio Mwenyekiti Mwenza wa maswala ya nishati safi ya kupikia .

Mkutano huu utaudhuliwa na mataifa mbalimbali kutoka duniani kote lengo kuu la mkutano ni kujadili sera,sheria,kanuni na taratibu zinazokwaimisha na kuludisha nyuma mipango ya nishati safi ya kupikia kwa nchi za Afrika ,pili kubolesha na kulekebisha sera,sheria,kanuni na taratibu zilizopo sasa na tatu kuzitaka nchi zilizoendelea na makampuni makubwa kutoa fedha na ahadi mbalimbali ambazo zitasaidia katika kuarakisha matumizi ya nishatisafi ya kupikia.

Waziri January Makamba amesema Tanzania imepata nafasi kubwa ya kushiriki mkutano huukwa sababu rais Dr Samia amekuwa kinara na ameweka mikakati mizuri na mikubwa katika kupigania matumizi ya nishati safi ya kupikia  Mkutano huu utafanyika tarehe 14 /5/2024 amesema haya jijini dar es salaam kwenye office ya mambo ya nnje.

Habari picha na Ally Thabit 


No comments:

Post a Comment