Saturday, 18 May 2024

MBIO ZA MSOGA HALF MARATHON KUOKOA MAISHA YA MAMA NA MTOTO


 Mratibu wa Mbio za Msoga Nelson Mrashana amesema mbio hizi zitafanyika tarehe 29/6/2024 wilaya ya Charinze eneo la Msoga  ,Lengo la mbio hizi kukusanya kiasi cha milioni Mia moja  ambako fedha hizi zitapelekwa kwenye hospital Msoga ili kuokoa maisha ya mama na mtoto wakati wa kujifunguwa hususani watoto ambao wanazaliwa kabla ya wakati (Njiti).

Pesa hizi zitasaidia kununua vifaa tiba mfano kangaroo . Nelson Mrashan amewataka watu binausi,taasisi,mashirika kushiriki kwenye mbio hizi ambako gharama za fomu elfu 35000 ambako fedha hizi unalipa kupitia lipa namba ya tigo 15840234 .

Habari picha na Ally Thabit 

No comments:

Post a Comment