Mtafiti kutoka Taasisi ya NIMR Tanzania amesema Tuzo alioipata leo nikwaajili ya tafiti anazozifanya zilivyoweza kusaidia mabadiliko kwenye sekta ya Afya ambako imepelekea mpaka kuwepo na mabadiliko makubwa ya kisera ambako apoawali kwenyesekta ya afya kuna sera zilikuwa zinakwamisha upatikanaji wa huduma bora za afya tanzania.
Pia ameandika Majarida ambayo yalizungumzia matatizo yaliopo kwenye sekta ya afya na kutoa mapendekezo na mabolesho ya sekta afya ,ambako serikali kupitia taasisi ya NIMR imefanyia kazi na kuleta mabadiliko kwenye sekta ya afya .
Dr Erizabeti Shayo ameweza kuwatia moyo wasichana na wanawake kushiliki kwenye maswala ya tafiti na kupenda masomo ya sayansi .ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwasomesha watoto wa kike kwani wanauwezo mkubwa wa kufanya kama rais Dr Samia. Amewataka kutenga muda wakuwa na familia pamoja na malezi pia washiliki katika shughuri mbalimbali za kiuchumi.
Swala la tafiti kuwafikia watu wenye makundi maalum ni muhimu na lina tija amesema haya kwenye kongamano la 32 la kisayansi lililoandaliwa na taasisi ya utafiti tanzania NIMR jijini dar es salaam ukumbi wa mwalimu nyerere.
Habari picha na Ally Thabit
No comments:
Post a Comment