Dr Doto Mashaka Biteko amesema tafiti zinazofanywa na National Institute for Medical Reseach (NIMR) zinasaidia kwa kiasi kikubwa katika kukuza sekta mbalimbali nchini tanzania Pia tafiti hizi zinawezesha serikali kufanya maamuzi sahihi kupitia tafiti zao na kupelekea kupatikana maendeleo kwa haraka na kwa kasi nchini tanzania .
Naibu Waziri Mkuu Dr Doto Mashaka Biteko amesema serikali itaendelea kutoa fedha nyingi kwenye National Institute for Medical Reseach (NIMR) wafanye tafiti zao za sayansi kwa kisasa kupitia teknolojia mpya kwani tafiti zao zimeboresha huduma za kiafya nchini na kupelekea kuwepo na madiliko ya sera za afya.
Pia serikali itaendelea kuboresha miundombinu kwenye mahabarata wanazofanyia tafiti na kuongeza wafanyakazi kwenye taasisi pamoja na kuboresha maslai yao.amesema haya kwenye kongamano la 32 lililojuisha watafiti wa kisayansi kutoka mataifa mbalimbali duniani ambako linafanyika jijini dar es salaam ukumbi wa mwalimu nyerere.
Habari picha na Ally
No comments:
Post a Comment