Taasisi ya NIMR Mkoa wa Mbeya inafanya tafiti kwenye magonjwa mbalimbali mfano marelia,ukimwi , Kifua kikuu ,kansa na magonjwa mengineyo Dr Lucas Maganga mtafiti taasisi ya utafiti NIMR Mbeya ameitaka jamii kuwa na uvumilivu kwa watu wanaofanya tafiti kwani tafiti autoi majibu ya hapo kwa hapo.
Ameitaka jamii watafiti wanapoenda kufanya tafiti zao wawape ushilikiano wa kutosha kwani utafiti unaitaji ushiliki mkubwa wa jamii , taasisi ya NIMR Mbeya inafanya kazi ya utafiti kanda ya kusini pamoja na mkoa wa mbeya kwa ujumla ambako mwaka1990 taasisi hii ilikuwa na mashilikiano na wabia kutoka ujerumani na marekani lakini ilipofika mwaka 2008 taasisi hii ya utafiti Mbeya ilichukuwa na taasisi ya utafiti NIMR ambako kwa sasa inatambulika taasisi ya utafiti NIMR Mbeya.
Dr Lucas Maganga amesema taasisi ya NIMR Mbeya imefanya tafiti za chanjo 10 za UKIMWI lengo kupata tiba na namna ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI kupitia chanjo hizi walizofanyia tafiti taasisi ya NIMR Mbeya inajumla ya wataalam 170
Kupitia Tafiti zao Wana Mipango na Mikakati ya kufikia makundi yote kwa sasa watu wenye uziwi wana mtaalam mmoja ambaye anatumia Lugha ya Alama, taasisi hii inasaidia serikali katika kufanya mabadiliko ya kisera kwenye sekta ya afya.
Habari picha na Ally Thabit
No comments:
Post a Comment