Inosendi Bashungwa waziri wa viwanda na biashara anaitaka tume ya ushindani kutokuwa na urasimu na kutokubali kuyumbishwa na wafanya biashara wakubwa katika kutekeleza majukumu yake Waziri amesma vitendo vya rushwa viongozi wa tume ya ushindani wasivikubali lengo watoe haki kwa wanyonge kwani tume imeanzishwa kwaajili ya kuleta usawa wa kishindani kwenye biashara
Ameipongeza tume kwa kumpa haki mfanya biashara mdogo wa sabuni ambae alikuwa ananyonywa na kugandamizwa na mfanya biashara mkubwa ambae aliiba rebo yake Inosendi Bashungwa ameupongeza uongozi wa tume ya ushindani kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa kuazimisha siku ya ushindani duniani ametoa wito kwa tume ya ushindani kutekeleza kwa vitendo ushauri,maoni na mapendekezo yaliotolewa kwenye kongamano la siku ya ushindani duniani amesema haya siku ya kilele cha ushindani viwanja vya mnazi mmoja jijini dar es salaam
Habari picha na Victoria Stanslaus
No comments:
Post a Comment