Mkurugenzi Mtendaji Tgnp Liliani Liundi amesema tarehe 19 ya mwezi 3 mwaka 2025 rais Dr Samia ametimiza miaka minne ya uongozi wake kitendo hiki wanaharakati wanaopigania haki za binadamu kwao ni mafanikio makubwa kwani watu wengi waliamini kuwa mwanamke awezi kuiongoza nchi . Kupitia rais Dr Samia zana hii mbaya na potofu dhidi ya mwanamke imeweza kufutwa na kunjwa.
Saturday, 22 March 2025
TGNP YAGUSWA NA UONGOZI WA RAIS DR SAMIA
UNDP YAIMIZA MIKAKATI IONGEZWE YA KUWAINUWA WANAWAKE
Mwakilishi wa Undp amesema Wanawake waweze kupewa fursa mbalimbali ili waweze kujikwamuwa kiuchumi hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na ukatili wa kijinsia .
Ndani ya miaka 30 ya Beijing wanawake wamejikomboa kiungozi, ardhi na wameweza kujiamini amesema haya viwanja vya tgnp mabibo katika siku ya mwanamke duniani na uzinduzi wa ripoti ya Beijing.
Habari picha na Victoria Stanslaus
BODI YA SUKARI YAJIVUNIA MAFANIKIO YA RAIS DR SAMIA KWA MIAKA MINNE
Prof Keneth Bengesi Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania amesema tangu tarehe 19 mwezi wa 3 mwaka 2021 baada ya Dr Samia kuapishwa na kuwa rais wa tanzania amewezesha sekta ya Sukari kukuwa na kupiga hatuwa kwa kuwapa ruzuku wakulima wa miwa, kwa kufanya mabadiliko ya sheria ya NFRA kwa kupewa mamlaka ya kuhifadhi Sukari ambako mwanzoni wafanyabiashara wa sukari walikuwa wanaifadhi wenyewe na kupelekea ufichaji wa sukari na kusababisha kupanda kwa bei ya sukari olela olela na kupelekea usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa sukari nchini tanzania.
Ujenzi wa viwanda vya sukari na upanuzi wa viwanda vya zamani vya sukari. Prof Keneth Bengesi amesema rais Dr Samia kwa kipindi cha uongozi wake wa miaka minne amekamilisha miradi yote ilioachwa na mtangulizi wake.mfano ujenzi wa bwawa la mwalimu nyerere, daraja la Kigongo busisi mwanza, ujenzi wa SGR, uwanja wa msarato jijini dodoma , amekuza demokrasia kwa kuwa nafasi viongozi wa vyama vya siasa kufanya mikutano yao kwa uhuru, maridhiano kwa kupitia farsafa yake ya R nne na kuwarejesha watu wote waliokimbia nje ya nchi.
Na mengineyo mengi ameyafanya rais Dr Samia ikiwemo kufunguwa fursa kwa wafabiashara, wasanii kwa kusafiri nao nje ya nchi kwaajili ya kuwatafutia masoko ya kitaifa na kimataifa , ameweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wawekezaji kuwekeza kwenye sekta ya sukari na maeneo mengineyo.
Ametoa wito kwa watanzania waendelee kumuunga mkono na mwaka huu kwenye uchaguzi wampe kura za kutosha rais Dr Samia ili aendekee kuwa rais wa Tanzania hakika rais Dr Samia mitano tena.
Habari picha na Victoria Stanslaus
MGENI RASMI AKIZINDUA RIPOTI YA TGNP
Mwenyekiti wa Jumuhiya ya Kiislamu na Waziri Msitaafu wa wizara ya viwanda na biashara na wizara ya maendeleo ya jamii , jinsia na watoto ambae alikuwa mbunge mwanamke kwanza kuchaguliwa na wananchi mnamo mwaka 1985 Hajati Shamimu pichani akizindua ripoti ya TGNP inayoeleza na kueleza hatua na changamoto zilizo jitokeza baada ya mkutano wa Beijing uliofanyika mwaka 1995 ambako kwa sasa tunatimiza miaka 30 ya Beijing.
Habari picha na Ally Thabit
HAJATI SHAMIMU AWAPONGEZA TGNP
Mwenyekiti wa Jumuhiya ya Wanawake wa Kiislamu Taifa na Mwana harakati mkongwe amewapongeza TGNP kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kupiga vita ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake , wasichana na makundi mengineyo na kupelekea idadi ya wanawake ya kuwa viongozi nchini tanzania imeongezeka. Mfano wabunge wanawake wa ku haguliwa wapo 26 ukilinganisha na miaka ya nyuma haya ndio walio yapigania kwenye mkutano wa Beijing nchini China mwaka 1995 amesema haya kwenye siku ya mwanamke duniani kwenye viwanja vya TGNP Mabibo jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally ThabitST. MATTHEW'S YAGUSWA NA MIAKA MINNE YA RAIS DR SAMIA
Wakiri Msomi na Mkurugenzi wa Shule za St. Matthew's Dr Peter Tadeo Mtembei amesema tarehe 19 mwezi wa 3 mwaka 2025 rais Dr Samia ametimiza miaka minne ya uongozi wake .Katika miaka hii amekuza na kustawisha maridhiano, miundombinu mfano ujenzi wa SGR,Barabara , Madaraja na Upatikanaji wa Maji safi na salama kwa wananchi wote.
Pia rais Dr Samia ameanzisha miradi mipya na kukamisha miradi ilioachwa na mtangulizi wake. kupitia sekta ya elimu amejenga madarasa mapya, mabweni, ameajili waalimu, ujenzi wa nyumba za walimu na mabadiliko ya sera ya elimu ambako inamuwezesha mwanafunzi akimaliza elimu yake anaweza kujiajili ama kuajiliŵa.
Vilevile Wakiri Msomi na Mkurugenzi wa Shule za St. Matthew's Dr Peter Tadeo Mtembei amewataka wa'azi na walezi kuwaandikisha watoto wao kwenye shule zote nane za St Matthew's kwani shule zao zinatoa elimu bora nidhamu na usalama ni vitu vya msingi na wanavizingatia na ufahuru wa uhakika na wakiwango cha juu.
Ametoa rai kwa wahitimu 97 wa kidato cha sita kwenye shule ya St. Matthew's iliyopo mkoa wa wa pwani wilaya ya mkuranga kata ya mwandege katika maafari haya ya 20 kwa mwaka 2025 pindi wa wakimaliza mitihani ya taifa wakawe mabalozi wema , waendeleze maadili mema kwa jamii, tabia njema na watumie elimu walioipata kutatuwa changamoto za kijamii.
Pia amewasisitiza wazazi na walezi kwa elimu bora, nidhamu na usalama kwa wanafunzi na gharama nafuu za ada ni vyema wachague shule za St Matthew's kwani kupitia Maendeleo Bank wazazi na walezi watakopeshwa ada kwa riba nafuu ya asilimia moja .
Habari picha na Victoria Stanslaus
MKUU WA WIRAYA YA KISARAWE AFUNGUWA MILANGO KWA WAZAZI NA WALEZI KWENYE SHULE YA ST MATTHEW'S
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Dr Tito Magoti anawataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kwenye shule za St. Matthew's kwani zinafundisha vizuri mpaka kupelekea mwanafunzi kuweza kujiajili kupitia mafunzo ya ujasilia Mali na kuondokana kuwa tegemezi katika jamii .
Shule za St. Matthew's zinaunga mkono na kutekeleza maono ya rais Dr Samia kwa kuwapa wanafunzi elimu bora na viwango vikubwa hivyo ni vyema wazazi na walezi wasiache kuwapeleka watoto wao kwenye shule za St. Matthew's.
Amesema haya kwenye maafari ya 20 ya kidato cha sita ambako wahitimu 97 wanamaliza elimu yao kwenye shule ya St. Matthew's wilaya ya Mkuranga kata ya mwandege mkoani pwani.
Habari na Ally Thabit
MAKAMU MWENYEKITI WA BODI YA SHULE YA ST. MATTHEW'S AFICHUWA SIRI NZITO
Makamu Mwenyekiti wa Bodi Shule ya St. Matthew's Dr Mwisiga amesema siri kubwa ya mafanikio kwa shule za St Matthew's katika wanafunzi kufahuru kwa kiwango kikubwa ni mazingira ni rafiki na wezeshi ya kufundishia na kujifunza wanafunzi.
Kuwepo kwa mahabara za kutosha na matumizi ya kiteknolojia ya kufundishia na kujisomea .swala la nidhamu, usalama na malezi ni misingi inayosimamiwa na kuzingatiwa kwenye shule zote za St. Matthew's.
Makamu Mwenyekiti wa Shule za St. Matthew's anawataka wazazi na walezi wawpeleke watoto wao kwenye shule za St Matthew's kwani watapata elimu bora na gharama ni nafuu na inalipika kwa hawamu nne lakini pia kupitia Maendeleo Bank watapata mkopo wa ada wenye riba ya asili moja .Makamu Mwenyekiti wa bodi Dr Mwisiga amesema swala la maadili, mafundisho ya dini , tabia njema ni vitu. Vinavyosimamiwa na kuzingatiwa kwa wanafunzi ndio maana ufahuru unaongezeka mwaka hadi mwaka amesema haya kwenye maafari ya 20 ya kidato cha sita kwa wanafunzi wapatao 97 wa shule ya St. Matthew's.
Habari na Ally Thabit
ST. MATTHEW'S INATOA ELIMU KWA GHARAMA NAFUU
Mkuu wa Shule ya St. Matthew's Josefu Malahila. amewataka Wazazi na walezi kuwahandikisha watoto wao kwenye shule zote nane za St. Matthew's kuanzia elimu ya Awali , msingi kwa Secondary kuanzia kidato cha kwanza mpaka kidato cha sita. Ambako mzazi analipa hada kwa awamu nne.
Shule za St. Matthew's zina malengo ya kutoa elimu inayozingatia nidhamu, usalama kwa wanafunzi na malezi bora kwa wanafunzi wote shule ya St Matthew's inamuwezesha mwanafunzi kujiajili ama kuajiliwa amesema haya kwenye maafari ya kidato cha sita ya wanafunzi wapatao 97 wa shule ya St.Matthew's.
Mkuu wa Shule ya St. Matthew's Josefu Malahila ametoa wito kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita elimu na ujuzi walioupata wakatumie katika kutatuwa changamoto za kijamii.
Habari na Ally Thabit
Wednesday, 19 March 2025
BALOZI RIBERATA MULAMULA AWATAKA WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA MBALIMBALI
Balozi Mulamula amewataka Wanawake Kuchangamkia fursa mbalimbali miongoni mwao zikiwemo fursa za kiuchumu ambako wakifanya biashara au ujasilia Mali watafanikiwa kiuchumi .
Pia amewataka wanawake wote wawe na elimu ya fedha amesema haya wakati wa kuwajengea uwezo wanawake na wasichana walipo kutana na Women Shaping the future (SRS) jijini dar es salaam.
Habari na Ally Thabit
SAMIA 4×4 WANAWAKE WAJAWAZITO WAGUSWQ NA SAMIA 4×4
Salmu Kikeke amesema Tarehe 5 ya Mwezi wa 4 mwaka 2025 amesema kutakuwa na msafara wa magari mia moja yataelekea mkoani Tanga eneo la pangani pia yatapita kwenye ushoroba wa saadani lengo ni kuonesha mafanikio na maendeleo yaliofanywa narais Dr Samia kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wake.
Samia 4×4 itagawa vifaa vya kujifungulia wamama wajawazito ambako vifaaa hivyo ni zaidi ya elfu moja ivyo wanawake wote wanatakiwa kujitokeza kwa wingi .
Pia msafara huu utapokelewa na waziri wa maji Awesu Juma Awesu .katika msafara huu kutakuwa na uzinduzi wa miradi mbalimbali iliyotekelezwa na rais Dr samia na kilele cha msafara huu wa Samia 4×4 utafikia tamati tarehe 8 mwezi wa 4 mwaka 2025.
Habari picha na Ally Thabit
MAENDELEO BANK YAJA NA CLICK BANK SMILE
Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo Bank Plc Prof Ulingeta Mbamba Azindua Huduma ya CLICK BANK SMILE amesema uzinduzi wa Internet Banking .
Amechukua fursa ya kuwapongeza kwa dhati Menejimenti na wafanyakazi wa Maendeleo bank kwa juhudi kubwa walizofanya kuhakikisha huduma hii mpya ya inakamilika na kuzinduliwa kwa mafanikio.jitohada,maarifa,na kujituma kwao kumeifanya Maendeleo bank kuwa kinara wa ubunifu katika sekta ya kifedha amewaponeza sana .
Katika Ulimwenngu wa sasa wa kidigitali,benkiinayoendelea ni ile inayokwenda sambamba na teknolojia- Click Bank Smile ni jibu sahihi kwa mahitaji yawateja wa leo wanaotaka huduma za haraka ,salama na zinazoweza kupatikana mahali popote na muda wowote .
Hivyo Matarajio ya huduma hii itaongeza ufanisi wa biashara, hasa kwa wafannyabiashaara wadogo na wa kati na kuokoa muda na gharama za wateja kwa kila kitu kinapatikana kwa mfuso wa kidole kwenye simu au kompyuta.
Huu ni ushahidi kwa Maendeleo Bank Plc inatekeleza kwa vitendo mkakati wake wa ukuaji wa kidigitali na kufanikisha azma ya kuwa benki ya kisasa inayoendana na mabadiliko ya kiteknolojia.
Kwa Mujibu wa Fin-Scope Survey ya Mwaka 2023 kiwango cha upatikanaji na matumizi ya huduma rasmi za kifedha kiliongezeka hadi 89% na 76% mwaka 2023 kutoka 86% na 65% mwaka 2017". Hii ilichangiwa sana na uimarikaji wa huduma za kifedha kwa njia ya kidigitali na hasa huduma za kifedha kwa njia ya simu.
Hivyo ni Imani kuwa huduma hii ya Internet banking si tu kwamba itawanufaisha wateja wa Maendeleo Bank tu bali pia itasaidia ukuaji wa uchumi wa wananchi kwa kuongeza ujumuishi wa kifedha nchini. Kwa namna hii, Maendeleo Bank inachangia moja kwa moja katika malengo ya serikali , katika kuimarisha uchumi wa kidigitali na kuhakikisha wananchi wengi wanapata huduma za kifedha kwa urahisi zaidi.
Pia ametoa wito kwa watanzania wote kutumia huduma hii ya CLICK BANK SMILE ili kujionea urahisi wake na manufaa yake .Hii ni huduma iliyoandaliwa kwa ajili yenu hivyo ni jukumu letu kuitumia kwa tija .
Kwa heshima na taadhima ,sasa ameitangaza rasmi kuwa huduma ya Internet banking ya Maendeleo Bank Plc -CLICK BANK SMILE- imezinduliwa rasmi, leo tarehe 18 mwezi wa tatu mwaka 2025 .PONGEZI KWA MAENDELEO BANK PLC!.
Habari na Ally Thabit
Tuesday, 11 March 2025
TAASISI YA BI AISHA SURURU YAAHIDI MAKUBWA KWA VIJANA
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Taasisi ya BI Aisha Sururu amesema wataendelea kuwawahifadhisha Quran vijana wote wa kitanzania na wasio watanzania lengo wamtambue mungu na wawe wenye maadili mama.
Monday, 10 March 2025
AMANA BENK YAAIDI MAZITO
Mkurugenzi wa Amana Benk Abubakari amesema watazidi kudhamini na kufadhiri mashindano ya Quran lengo kuwatia moyo wanaohifadhi na kusoma Quran na kukikuza kitabu cha mungu amesema haya kwenye mashindano ya 25 ya kuifadhi Quran yalioandaliwa na taasisi ya Bi Aisha Sururu foundation ambayo yamefany8ka jijini dar es salaam.
Habari picha na Victoria Stanslaus
BI ASHA DIWANI VITI MAALUM JIJI LA ILALA AIMIZA WAZAZI NA WALEZI KUWAPELEKA WATOTO WAO KUSOMA QURAN
Diwani wa Viti Maalum na Mweka hazina kwenye taasisi ya Aisha Sururu Foundation anawataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kusoma Quran kwani kuna faida zinapatikana zikiwemo kuwa na imani,kuulumia binadamu mwenzako,kuwana ofu na kuwa mwadilifu na weredi katika kazi na jamii kwa ujumla .
Habari picha na Victoria Stanslaus
MJUMBE WA ALMASHAURI KUU YA CCM APONGEZA MASHINDANO YA QURAN
Amoll Abudi Juma Mjumbe wa Almashauri Kuu ya ccm taifa mkoa wa dar es salaam amempongeza bi Aisha Sururu kwa kuendesha mashindano ya quran kwa miaka ishilini na tano pamoja na kuwahifazisha maneno ya mungu watoto yatima,wajane,wasiojiweza,watu wa makundi maalum kwani kufanya hivi kunasaidia kupata watu wenye maadili,wenye ofu ya mungu na hatimae nchi ya tanzania inapata amani ,upendo na utulivu.
SHEIKH PONDA AELEZA UMUHIMU WA FUNGA
Sheikh Issa Ponda amewataka Waislamu wote wale ambao awana matatizo ya kiafya waweze kutekeleza nguzo ya nne ya kiislam kati ya tano wafunge ramadhani ndani ya mwezi huu wa ramadhani kwani watakuwa waja wema pia wasome Quran mara kwa mara.
Habari na Victoria StanslausSHEIKH CHIZENGA AELEZA FAIDA ZA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI
Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Ulamaa Bakwata amewataka waislamu nchini tanzania wafunge ramadhani kwenye mwezi huu mtukufu wa ramadhani kwani miongoni mwa faida watakazozipata ni kuimarika kwa afya zao .Pia mungu atawasamehe makosa yao na zambi zao pia anawasisitiza watanzania wote bila jujali dini,kabila,rangi na jinsia wazidi kumuombea afya njema rais Dr Samia kwani amekalisha miradi yote na anatenda haki kwa kila mmoja hivyo ni vyema kumchagua kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu hakika mama samia mitano tena.
Habari picha na Ally Thabit.KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI AWATOA OFU WATANZANIA
Wednesday, 26 February 2025
MKURUGENZI AIMIZA MIFUMO YA MITAJI YA MASOKO YA ISA HIIMARISHWE
Mitaji ya Masoko ya Isa Ikihimarishwa Idadi ya Wawekezaji itaongezeka ambako kwa sasa watu laki6 wamewekeza kwenye masoko ya isa Cipiey Nikolaus ameipongeza kampuni ya VERTEX INTERNATIONAL SECURITIES LTD kwa kusimamia fedha za wawekezaji.
Habari picha na Ally Thabit
Saturday, 22 February 2025
MSANII JEYB AWATAKA WASANII KUMUUNGA MKONO RAIS DR SAMIA
Barozi wa Chama cha Ccm Msanii Jeyb anawata wasanii nchini tanzania kujiunga na chama cha ccm na kumuunga mkono rais Dr Samia kwani ameweza kutekeleza kwa vitendo miradi yote ya kimkakati mfano ujenzi wa SGR ,amewapa wasanii mikopo ya fedha ambayo aina riba bila kujali chama dini wala rangi na jinsia .
Barozi Jeyb amesema watafanya kampeni nchi nzima ya kuakikisha watu wanajiunga na chama cha ccm na rais Dr Samia anashinda kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Habari picha na Ally Thabit
KATIBU MKUU NA MSEMAJI WA SERIKALI ABAINISHA MIKAKATI YA WAKULIMA WA KAHAWA
Greyson Msigwa Katibu Mkuu na Msemaji wa Serikali amesema kuwa serikali ya tanzania imeweka mazingira rafiki na wezeshi kwenye zao la kahawa kwa kuwapa wakulima wa kahawa pembejeo zenye ubora na za kisasa ,Mbegu zenye ubora,Mafunzo kwa wakulima wa kahawa,Teknolojia za kisasa na zenye ubora na kufanya tafiti pamoja na kuwatafutia masoko wakulima wa kahawa ndani ya nchi na nje ya nchi.
Lengo la kufanya haya yote ni kuwainuwa wakulima wa kahawa kiuchumi na kuongeza uzalishaji wenye tija katika kahawa . Baada ya serikali kuyafanya haya yote chini ya rais Dr samia hatimae kahawa ya tanzania imepanda thamani kubwa na kupelekea kahaya ya tanzania kuuzika katika masoko ya kitaifa na kimataifa .
Katibu Mkuu na Msemaji wa Serikali amesisitiza kuwa watu wenye ulemavu katika zao la kahawa wanashirikishwa kikamilifu Pia kupitia mradi wa BBT watu wenye ulemavu wapo na kupitia mikopo ya halmashauri watu wenye ulemavu wanapewa pesa kwaajili ya kufanya biashara mbalimbali amesema haya kwenye mkutano 3RD G25 AFRICAN SUMMIT 2025 uliofanyika jijini dar es salaam.
Habari picha na Ally Thabit Mbungo
Friday, 21 February 2025
WAZIRI WA KILIMO AZITAKA NCHI ZA AFRIKA KULETA MAGEUZI KWENYE ZAO LA KAHAWA
Husen Bashe Waziri wa Kilimo anazitaka Nchi zote za bara la Afrika kuweka mkazo mkubwa kwenye zao la kahawa kwa kutenga bajeti za kutosha kwaajili ya kununua pembejeo,Kuweka program kwa wakulima wa kahawa ,Kuwatafutia masoko ya kimataifa na kuwawezesha teknolojia za kilimo amesema haya kwenye mkutano wa 3RD G25 African Coffee Summit 2025 unaofanyika jijini Dar es salaam.
Habari na Ally Thabit
ANT EZEKIEL AJIUNGA NA CHAMA CHA CCM
Msanii Ant Ezekiel ameamuwa Kutoka chama cha Chadema na kujiunga na chama cha ccm kwani rais Dr samia anawaunga mkono wasanii kwa kiasi kikubwa kwa kuwapa mikopo na kuweka mazingira rafiki kwa wasanii na ameahidi atakuwa balozi wa chama cha ccm.
STAMINA KUMLUDISHA ROMA TANZANIA
Msanii wa Kizazi Kipya Stamina na balozi wa chama cha ccm amesema atamshawishi msanii Roma aliopo mafichoni nchini marekani aweze kurudi nchini tanzania na kujiunga na chama cha ccm.
Habari picha na Ally Thabit
TANTRADE YAJIVUNIA NA TUZO
Ratifa Mohamed Mkurugenzi wa TANTRADE amesema tuzo zitasaidia kuwakuza wafanyabiashara wadogo na wakati kwani biashara zao watazalisha bidhaa zenye ubora na watazingatia alama zote.
Habari na Ally Thabit
MWENYEKITI WA CHAMA CHA KAHAWA WA AFRIKA APONGEZA MKUTANO WA WADAU WA KAHAWA
Mwenyekiti wa Chama cha Kahaha bara la Afrika amesema mkutano wa wadau wa kahawa utasaidia kuweka sera na sheria katika kukuwa kwa zao la kahawa na kutatuwa changamoto la zao la kahawa.
Habari picha na Ally Thabit
Saturday, 8 February 2025
MKURUGENZI MKUU MTENDAJI WA HOSPITALI YA OCEANROAD CENCER INSTITUTE AMSHUKURU RAIS DR SAMIA
Diwani Othman Msem Mkurunzi Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya OCEAN ROAD CANCER INSTITUTE anamshukuru rais Dr Samia kwa kuweza kununua mashine mfano MRI na zinginezo kwaajili ya kufanya uchunguzi na tiba kwa nagonjwa ya saratani za aina zote . Pia anashuru kwa kuweza kutoa pesa nyingi kwaajili ya kununua dawa kwa wagonjwa wa saratani .
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji Diwani Othman Msem anawataka watu kufanya uchunguzi wa miili yao lengo wakugundulika na saratani waanze matibabu mapema kwani saratani inatibika . Ameishukuru Gsm Foundation kwa jitihada kubwa wanazozifanya za kuzibiti na kupambana ili kutokomeza saratani za aina zote kwa kutoa michango ya pesa,mawazo,elimu na vitu mbalimbali kwa kushirikiana na hospitali ya Ocean road cancer Institute.
Amesema haya siku ya saratani duniani kwenye hospitali ya Ocean road cancer Institute ambapo uazimishwa kila ifikapo tarehe 4 ya mwezi wa 2 duniani kote .
Habari na Ally Thabit
Friday, 7 February 2025
MASHUJAA WA SARATANI PAMOJA NA WADAU WANAOPIGA VITA SARATANI ZA AINA ZOTE WAPO KWENYE MATEMBEZI
FAITH GUGU MKUU WA GSM FOUNDATION AAHIDI MAKUBWA KWENYE HOSPITALI YA OCEANROAD CENCER INSTITUTE
Mkurugenzi Mkuu wa GSM FOUNDATION Faith Gugu amesema wataendelea kushirikiana na hospital ya Ocean road Cancer Institute katika mapambano ya saratani za aina zote lengo kutokomeza au kupunguza uogonjwa wa saratani na vifo vinavyotokana na saratani za aina zote kwani GSM FOUNDATION inatoa elimu kwa jamii ya kujilinda dhidi ya magonjwa ya saratani. Elimu hii inawafikia watu wenye ulemavu wa aina zote.
Amesema haya kwenye kilele cha maazimisho ya saratani yalio fanyika kwenye Hospitali ya Ocean road cancer Institute ambako uazimishwa kila tarehe 4 ya mwezi wa 2 duniani kote kila mwaka .
Habari na Ally Thabit
GLORIA KIDA MKURUGENZI WA ASASI YA SHUJAA WA SARATANI AIMIZA WATU KUPIMA SARATANI
Mkurugenzi wa Asasi ya Shujaa wa Saratani Gloria Kida anawataka watu kujitokeza kwa wingi kupima saratani za aina zote Pia anawahimiza wanajamii kuchanja chanjo ya HPV wao na watoto wao kwani ni kinga dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi .
Asasi yao Imetoa Elimu ya Saratani Katika Mkoa wa Mwanza na Wilaya zote za Dar es salaam amesema haya kwenye kilele cha week ya saratani iliyo fanyika kwenye Hospitali ya Oceanroad Cancer Institute ambako kila mwaka uazimishwa tarehe 4 ya mwezi 2 duniani kote .
Habari na Ally Thabit.
ASCP MULIRO J. AELEZEA WATOTO WALIOJITEKA
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Limewapata na Kuwahoji wasichana wawili ambao ambapo mmoja wa miaka16 Mwanafunzi wa kidato cha pili na mwingine wa miaka 12 Mwanafunzi wa Darasa la saba wakazi wa vijibweni kigamboni kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo baada ya kutengeneza mazingira kuwa wametekwa na watekwaji wanataka pesa.
Ufuatiliaji ulifanywa na kufanikiwa kubainiwatoto hawa walipokuwa na baada ya mahojiano ya kina walikiri kutengeneza tukio hili la uongo ili waweze kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu toka kwa wazazi wao baada ya kutoweka tarehe 26/01/2025 na kuelekea Longoni Beach ambapo walikesha hapo hadi tarehe 27/01/2025 asubuhi na baadae kuelekea maeneo ya Tungi hadi walipo kamatwa wakiwa wanazunguka. Jeshi linalaani vitendo vya hivi vya watu wenye lengo la kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu.
Aidha, Jeshi la Polisi Kanda ya Maalum Dar es salaam katika kipindi cha Desemba hadi Januari 2025 katika kusimamia mifumo ya haki jinai mahakamani baadhi ya watuhumiwa mbalimbali walipatikana na hatia ikiwa ni pamoja na Idrisa Rasshid miaka [35] Mkazi wa Kwembe Kimara alihukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kubaka kwenye Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni. Paul Elisha miaka (37) mkazi wa Mbezi Beach kwe nye Mahakama ya Kinondoni alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka na Jackson Mgeta (34) mkazi wa Kawe alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka.
Jeshi la Polisi lina wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana ili kuimarisha mifumo ya ulinzi shirikishi ikiwa ni pamoja na kutekeleza falsafa ya ulinzi shirikishi ili kuzuia vitendo vya kihalifu. Imetolewa na Kamanda Kanda Maalum ya Polisi Dar es salaam.
Habari na Ally Thabit Mbungo.