SEBASTIAN MROPE MSIMAMIZI WA TEKNOLOJIA NA UBUNIFU SIDO
Amesema katika kumuunga mkono Raisi Samia Suruhu Hassan SIDO inafanya ubunifu wa Teknolojia Mbalimbali zikiwemo Teknolojia ya usindikaji wa mazao ya kilimo kwa kubuni mashine mbalimbali, pia SIDO inatoa elimu kwa watanzania namna ya kuunda na kutengeneza mashine.
Mpaka sasa SIDO inavituo vya kuendeleza Teknolojia kwenye Mikoa Saba ikiwemo Mkoa wa Lindi ambako kuna machine za kubwangua korosho, kusindika mihogo, na Chumvi, Pia Iringa Kuna mashine za mafuta za mbegu mbalimbali, Mbeya kuna mashine za mahindi, Kigoma kuna mashine za kutengeza mafuta ya mawese, Arusha Mashine za Mbao, Shinyanga Mashine za Ngozi na Kilimanjaro mashine za matunda.
Sebastian Mrope amesema lengo la SIDO kuwasaidia watanzania waweze kutengeneza bidhaa bora ili wajikwamue kiuchumi. Hivyo amewataka watu kutembelea banda la SIDO kwenye maonyesho ya 45 viwanja vya sabasaba.
habari picha na Ally Thabith
No comments:
Post a Comment