Thursday, 16 July 2020

ALLY THABITI AINGIA KWENYE KINYANG'ANYILO CHA UCHAGUZI

Ally Thabiti no Kijana Mwenye Ulemavu wa Kutokiona ameamuwa kuchukua fomu kupitia Chama cha Mapinduzi CCM kwaajili ya kugombea Udiwani katika kata ya Kijichi Wilaya ya Temeke Jimbo la Mbagala Mkoa wa Dsm .amesema Lengo lake kwenda kusimamia asilimia 2 ya fedha kwenye Halmashauri zitengwe na wapewe watu wenye Ulemavu na kusimamia bajeti yenye Malengo wa wa kijinsia katika Halmashauri na ujenzi wa mabweni kwaajili ya wanafunzi wa kike pamoja na kusimamia makundi mengineyo Ally Thabiti amehaidi akipewa nafasi ya kuwa Diwani atasimamia na kutekeleza Kwa Vitendo maswala ya kupinga rushwa,ufisadi,ubadhirifu na kuamasisha watu waliojiajili kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii hasa NSSF .Pia amempongeza rais Magufuli Kwa utendaji wake wa kazi ulio tukuka na Asasi za kiraia ikiwemo TGNP MTANDAO,THRDC na zinginezo Kwa kutoa Elimu

Habari picha na Victoria Stanslaus

No comments:

Post a Comment