Wednesday, 15 July 2020

MWANAMAMA AJITOSA KUGOMBEA URAISI KUPITIA ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE(ADC)

            Mh, Doyo hassani Doyo( Kulia)
       Katibu mkuu wa chama cha ADC
Wakati wa uchukuaji fomu kuteuliwa kugombea uraisi wa chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Mwamama Mh Queen Cuthbert sendiga amejitokeza kuchukua fomu hiyo ili kupeperusha Bendera ya chama hicho katika kinyang'anyiro cha uraisi kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika October mwaka huu
Katibu Mh Doyo akieleze mikakati yao mikuu amesema, kwanza kabisa watasimamisha wagombea ubunge majimbo 100  ili walau waweze kuchukua majimbo 20 au 15 katika uchaguzi ujao
Amesisitiza kuwa chama chao kitajikita zaidi vijijini ili kutafta kura mpya ambazo si za chama chochote. Akifafanua kwa kurejea takwimu za uchaguzi uliopita amesema kura milioni 8 zilienda CCM na kura miliono 6 zilienda CHADEMA hivyo wao watatafuta kura milioni 9 ambazo ziliachwa na vyama vingine vyote
Mgombea uraisi Mh Queen Cuthbert pia amekili kuwa Mh JP Magufuri amefanya mengi mazuri ingawa si vyakutosha. Ataenda kuhakikisha
 -Vijana wanapata ajira vyakutosha ili waweze kujikwamua katika umasikini
 -Uchumi wa mtu mmoja mmoja
 - kuinua kilimo ili kupata bidhaa nyingi sokoni na viwandani
 -Kujenga madarasa ya kutosha ili kukuza elimu na kufuta kabisa ujinga
Mgombea uraisi ADC mama Queen Cuthbert Sendiga
HABARI PICHA NA ALLY THABITI

No comments:

Post a Comment