Kamishina Joachim Mahega amesema ameamuwa kuchukua fomu ya kuwania Ubunge jimbo la Kibaha mjini kwa tiketi ya NCCR Mageuzi lengo atatue matatizo makubwa na mazito yanayowasibu wana Kibaha mjini kwani inamuuma na kumgusa wakina mama wanavyopoteza maisha wakati wa kujifungua huku watoto wa kike wakikosa furusa ya Elimu na vijana pamoja na wazee kukosa shughuri za kujipatia kipato . Amewasii na kuwaasa wamchague yeye ifikapo tarehe 28 mwezi 10 2020 kupitia NCCR Mageuzi awapiganie na awatatulie matatizo yao
Habari picha na Victoria Stanslaus
Habari picha na Victoria Stanslaus
No comments:
Post a Comment