James Kilaba Mkurugenzi Mkuu wa Mamraka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) amesema tupo duniani Kwa mapenzi ya Mungu ivyo amewataka wanahabari,wanasiasa na watu wengine kulinda na Kuitunza Amani tulio nayo kipindi hiki cha Uchaguzi na Kampeni Tanzania
. Amesema TCRA imetoa leseni Kwa vyombo vya habari Lengo waelimishe jamii ,watoe ujumbe ,waburudishe na waweze kuwapa habari watu hivyo amewataka Wana habari na wamiriki wa vyombo vya habari wazingatie na kufuata taratibu, kanuni na Sheria za Mahudhui ya leseni zao Pia amewataka kuzingatia kanuni za Uchaguzi za mwaka 2015 kanuni ya 39 na vifungu vyake ambako Tume ya Uchaguzi Tanzania ndio yenye Mamlaka ya Kutangaza na kutoa taarifa za ushindi wa Wagombea Kwa ngazi zote za Uchaguzi amesema haya wakati akiongea na Wana habari wakati akitoa taarifa za kikifungia kituo cha Clauds Midia upande wa Redio na TV kuanzia tarehe 28 Mwezi 8 mpaka tarehe 3 Mwezi wa 9 Kwa kutotoa huduma zozote za matangazo baada ya kukiuka kanuni za Mahudhui za TCRA na Kanuni za Uchaguzi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi TanzaniaHabari picha na Ally Thabiti
No comments:
Post a Comment